USIUZE KADI YAKO

USIUZE KADI YAKO

Focusradiotz

Alhamisi, 3 Septemba 2015

UWEKAJI WAZI DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA MKOA WA DAR ES SALAAM

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

YAH: UWEKAJI WAZI DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA MKOA WA DAR ES SALAAM

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekua ikiendesha zoezi la Uwekaji wazi Daftari la awali la Wapiga Kura katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Zoezi hili ambalo lilianza tarehe 19 Agosti, 2015 linatarajiwa kumalizika Tarehe 07 Septemba 2015
Daftari la awali la Wapiga Kura limewekwa wazi katika kata zote za jiji la Dar es Salaam.  Mashine za BVR zinazotumika kufanyia marekebisho zimewekwa katika kata zote za jiji la Dar es Salaam.

Uwekaji wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura unahusisha mambo yafuatayo:
·      Kurekebisha taarifa za Mpiga Kura zilizokosewa wakati wa uandikishaji.
·      Kutoa kadi mpya kwa wapiga kura waliopoteza kadi zao na wamo katika Daftari la awali la Wapiga Kura. 
·      Kuondoa Wapiga Kura waliofariki au waliokosa sifa kwa mujibu wa sheria.
·      Kuhamisha taarifa za wale waliohama toka Kata au Jimbo kwenda Kata au Jimbo lingine.
·      Kutoa nafasi kwa wapiga kura walioandikishwa kukagua taarifa kama zipo kwenye Daftari.
·      Wale ambao wana kadi za Mpiga Kura lakini majina yao hayaonekani katika Daftari la Awali la Wapiga Kura watafanyiwa uhakiki katika mifumo ya BVR na iwapo itathibitika kuwa wamo watarudishwa katika mfumo wa Daftari.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inategemea ushirikiano wenu katika kufanikisha zoezi hili kwa kuwafahamisha wananchi ratiba ya zoezi hili na kuwahamasisha ili waweze kujitokeza kwa wingi

NB:   Unaweza kukagua taarifa zako kwa njia ya simu kwa kubonyeza *152*00≠ au tovuti www.nec.go.tz na kufuata maelekezo



Kailima, R. K

MKURUGENZI WA UCHAGUZI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni