USIUZE KADI YAKO

USIUZE KADI YAKO

Focusradiotz

Ijumaa, 30 Oktoba 2015

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva amkabidhi hati ya Ushindi Rais na Makamu wa Rais Mteule katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.


  Rais Mteule wa awamu ya tano, Dk. John Magufuli akiyonyesha hati ya ushindi wa Urais, baada ya kukabidhiwa leo na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva, katika hafla ya kukabidhi hati hiyo iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Dk. Magufuli amekabidhiwa cheti hicho kufuatia kuibuka mshindi wa kiti cha Urais katika matokeo yaliyotangazwa na NEC, ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu. Kushoto ni Makamu wa Rais Mteule, Mama Samia Suluhu Hassan.
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva akimkabidhi hati ya Ushindi Makamu wa Rais Mteule, Mama Samia Suluhu Hassan, katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Dk. John Magufuli

 Rais Mteule wa Tanzania, Dk. John Magufuli akipongezana na Makamu wake pia Mteule, Mama Samia Suluhu Hassan, baada ya kukabidhiwa hati zao za ushini na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Msaafu Damaian Lubuva, leo Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu, Damian Lubuva akiwapongeza Rais Mteule Dk. Magufuli, na Makamu wake Mteule,
  Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Rais Mteule, Dk. John Magufuli, baada ya kukabidhiwa hati ya ushindi wa kiti cha Urais 
  Rais Mteule Dk. Magufuli akimpongezwa na Mkewe Mama Jannet Magufuli, baada ya kukabidhiwa hati ya ushindi wa Urais. Kushoto ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete. na kulia ni Makamu wa Rais Mteule  Mama Samia Suluhu Hassan

  Dk. Magufuli akionyesha hati yake kwa wananchi baada ya kukabidhiwa hati hiyo  Picha ya Pamoja, Dk. Magufuli na Viongozi wa dini waliohudhuria
Picha zote kwa hisani ya
http://abdallahmrisho.blogspot.com/2015/10/dk-magufuli-akabidhiwa-cheti-chake-cha.html