USIUZE KADI YAKO

USIUZE KADI YAKO

Focusradiotz

Jumatano, 7 Oktoba 2015

Wasimamizi wa Uchaguzi toka majimbo yote nchini wakutanishwa Jijini Dar es Salaam.

Wasimamizi wa Uchguzi nchini wametakiwa kusimamia sheria katika kutekeleza majukumu ya kusimamia Uchaguzi unaotarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

Mwenyekiti wa Uchaguzi Jaji mstaafu Damiani Lubuva amesema hayo katika hotuba ya ufunguzi kwa Wasimamizi wa Uchaguzi toka majimbo yote nchini kwa lengo la kupata uzoefu kuboresha utendaji kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao.
“Mpaka sasa zoezi la kampeni linakwenda vizuri tufanye kazi zetu kwa weledi, kila mmoja wetu ashiriki kikamilifu katika mkutano huu, ili kuweza kupata michango itakayoweza kufanikisha uchaguzi huru, haki na amani ukizingatia kwamba wengi wenu ni wazoefu, kupitia wakati huu mtaweza kushirikishana uzoefu na kujifunza”

Aidha Lubuva ameongeza kuwa NEC imehusisha jeshi la polisi kwa lengo la kupata maoni yao ya namna ya kusimamia Uchguzi na kuwataka washiriki wote kutambua kuwa wanajukumu kubwa la kuhakikisha amani inakuwako na itaendelaa kuwako hata baada ya `uchaguzi.

Wakurugenzi hao wametakiwa kutomruhusu mtu au kikundi cha watu, vijana kusimama karibu na vituo vya kupigia kura kwa madai ya kulinda kura hii ni kukiuka taratibu na sheria na kuwasihi wawe na ushirikiano na kuwa karibu na NEC wakati wote wa shughuli za Uchaguzi kwa lengo la kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani nchini.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni