USIUZE KADI YAKO

USIUZE KADI YAKO

Focusradiotz

Alhamisi, 30 Julai 2015

NEC YAONGEZA SIKU NNE ZA KUANDIKISHA WAPIGA KURA JIJINI DAR ES SALAAM

Tume ya Uchaguzi (NEC) leo imetangaza kuongeza siku nne zaidi za uandikishaji wa wapigakura kwa kutumia teknolojia ya BVR baada ya idadi kubwa ya wakazi wa Dar es Salaam kuitikia wito wa zoezi hilo. 

 Awali zoezi hilo lilikuwa likamilike kesho, Julai 31, lakini sasa litaendelea hadi Agosti 4, mwaka huu ili kukabiliana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza kujiandikisha. 

Kwa mujibu wa chombo hicho chenye mamlaka ya kusimamia shughuli zote za uchaguzi nchini, hadi jana, zaidi ya wakazi 1,000,000 walikuwa wamekwishaandikishwa jijini Dar es Salaam. 

 Ikizingatia matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Nec inatarajia kuandikisha jumla ya wakazi zaidi ya 2.8 milioni wa jiji hilo lenye idadi kubwa ya watu nchini Tanzania. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva, hadi sasa jumla ya zaidi ya watu 18 milioni wamekwishajiandikisha wakati tume ilitarajia kuandikisha watu kati ya 22 milioni na 23 milioni.

JAJI MUTUNGI AJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGAKURA

MU1
Mhe. Jaji Francis S.K. Mutungi akiwa na kitambulisho chake mara baada ya kujiandikisha mapema Leo katika kituo cha Shule ya Msingi Bunge Jijini Dar es salaam.
MU2
Mwandikishaji Msaidizi Bi. Maida Ally Yusufu akimsainisha Jaji Mutungi  fomu ambazo zimebeba taarifa zake kwa ajili ya kujiandikisha Leo katika kituo cha Shule ya Msingi Bunge Jijini Dar es salaam
MU3
Alama za vidole zikichukuliwa na Mwandikishaji Bw. Ernest Moses Selelya mara baada ya kukamilisha taratibu za ujazaji wa fomu ya utambulisho.
MU4
Jaji Mutungi akipiga picha kwa ajili ya kitambulisho.
MU5
Mhe.Jaji  Francis Mutungi akipokea  kitambulisho cha mpiga kura kutoka kwa Mwandikishaji Bw.Ernest Moses Selelya.

Jumatano, 29 Julai 2015

NEC YAKUTANA NA UONGOZI WA MKOA WA DAR ES SALAAM KUTATHIMINI ZOEZI ZIMA LA UANDIKISHWAJI BVR

 Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekutana na viongozi waandamizi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na mkuu wa mkoa huo, wakuu wa wilaya zote na wakurugenzi wa manispaa zote kutathimini hali ya zoezi zima la uandikishwaji mkoa wa Dar es salaam.

 Pamoja na changamoto zilizoainishwa ikiwemo rasimali Fedha yalijadiliwa kwakina,Tume imetoa wito kwa uongozi wa Dar es salaam kuhakikisha matatizo yaliyoainishwa yanatatuliwa katika siku zilizobaki ikiwemo uhaba wa watumishi vituoni suala la rushwa,na taarifa za mahitaji ya BVR kwa wakati kwani mashine hizo zipo za kutosha. 
  Serikali Pia imekwisha Toa madai yote ya kila mnispaa yaliyokuwa kikwazo katika zoezi zima linaloendelea mkoa wa Dar es Salaam ikiwemo rasilimali fedha. 

 Akiongea na waandishi wa Habari M/kiti wa Tume Jaji wa Rufaa mstaafu Damian Lubuva amesema hakuna mkazi yoyote hata andikishwa Dar Es salaam. Amewataka Wanahabari kuhakikisha wanakusanya taarifa sahihi kwa wakati na kuuelimisha umma wa Watanzania maswala yote yanayohusu Uandikishwaji na upigaji kura

UANDIKISHAJI JIJINI DAR ES SALAAM

MWENYEKITI WA NEC JAJI MSTAAFU DAMIAN LUBUVA AZUNGUMZA NA WAANDISHI

NEC YAREKEBISHA KASORO CHACHE ZA UANDIKISHAJI KWA BVR JIJINI DAR ES SALAAM

 Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damiani Lubuva, akizungumza na waandishi wa Habari mapema wiki hii Katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
  Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damiani Lubuva, akijiandikisha katika Daftari la kudumu kwa mfumo wa BVR mapema wiki hii.
 Baadhi ya wananchi wa jijini Dar es Salaam wanaoendelea kujitokeza ili kujiandikisha kwa mfumo wa BVR.

DAFTARI LA AWALI LA WAPIGAKURA LAENDELEA KUCHAPISWA

 Mkurugenzi wa Uchaguzi mpya Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey usiku wa Tarehe 28/7/2015 akijionea hatua mbali mbali za uchapishaji wa Daftari la awali la wapigakura.
Tayari usambazaji katika mikoa sita umekwisha fanyika ikiwa ni Iringa, Mtwara, Njombe, Lindi, Rukwa na Mbeya kwa wananchi kuhakiki taarifa zao katika daftari la awali 'nataka hadi wiki ijayo tuwe tumebakiza Dar es Salaam tu sawa jamani, niambieni mapungufu yetu na asubuhi kesho tunayatatua kazi iende alisikika akiwaelekeza watendaji usiku ule hakuna kulala hapa kwa gharama yoyote alibainisha.
Taarifa za kuanza kwa uhakiki wa daftari la awali katika mikoa iliyosambaziwa zitatolewa punde katika mikoa husika kwa vyombo vya habari.Ni muhimu kuhakikisha Taarifa zako baada ya kujiandikisha.

Jumatatu, 13 Julai 2015

MAJIMBO 26 MAPYA YA UCHAGUZI BAADA YA KUGAWAMYWA

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza majimbo mapya ya uchaguzi katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. 
--- 
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza majimbo 26 mapya ya uchaguzi ambayo yatakuwa na wagombea katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu. 

 Akizungumza na waandishi wa habari leo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kukata kwa majimbo hayo wamezingatia idadi ya watu pamoja na Jiografia katika majimbo mapya. 

Amesema katika upande wa Zanzibar majimbo yamebaki kuwa 50 kama awali hiyo inatokana vigezo vilivyowekwa na tume hiyo. Majimbo yaliongezwa ni Handeni Mjini, Nanyamba, Makambako, Butiama, Tarime Mjini, Tunduma, Msimbo, Kavu, Geita Mjini, Mafinga Mjini, Ushetu, Nzega Mjini, Kahama Mjini, Kondoa Mjini, Newala Mjini, Bunda Mjini, Mbulu Mjini, Ndanda, Madaba, Mbinga Mjini, Mbagala, Kibamba,Vwawa,Monongo,Mlimba, Pamoja na Uliambulu. 

 Jaji Lubuva amesema baadhi ya wabunge wamekuwa wakiingia katika Halmashauri mbili hiyo kuweka mipaka katika maeneo ili mbunge aweze kushiriki katika Halmashauri moja tu. Amesema baadhi majimbo yamebadilishwa majina na kuendelea kuwepo kwa majimbo hayo kisheria.

VIDEO MPYA NEC PWANI 07mpaka20JULAY &DAR ES SALAAM 22 Mpaka 31 ULY TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI 2015

Jumanne, 7 Julai 2015

ZOEZI LA UBORESHWAJI DAFTARI LA WAPIGAKURA LAENDELEA MKOANI PWANI, RAIS JAKAYA KIKWETE AJIANDIKISHA KUPIGA KURA KWA KUTUMIA BVR KIJIJINI MSOGA

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo mpya wa kielektoniki(Biometric Voters Register( BVR) katika kijiji cha Msoga,kata ya Msoga wilayani Bagamoyo leo.Kulia akiangalia kwa makini ni mwandikishaji msaidizi Bi.Happyness Thomas Misana na katikati ni Afisa TEHAMA kutoka ofisi Tume ya Taifa Uchaguzi Bi.Mariam Rajabu.Kushoto aliyesimama akishuhudia ni Mbunge wa Chalinze Ridhwani Kikwete.
 Afisa TEHAMA kutoka ofisi ya Tume ya Uchaguzi Taifa ya Uchaguzi Bwana Sanif Khalfan akichukua lama za vidole vya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipokwenda kujiandikisha kijijini kwake Msoga wilaya ya Bagamoyo leo .
 Bwana SANIF Khalfan ambaye ni Afisa TEHAMA kutoka ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi akimpiga picha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipokwenda kujiandikisha kupiga kura kwa kutkumia teknolojia mpya ya BVR kijijini Kwake Msoga leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitambulisho chake wakati wa zoezi la kujiandikisha kijijni kwake Msoga leo.
 Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kitambulisho chake cha kupiga kura baada ya Rais Kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo.
Rais Kikwete akimshukuru Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva baada ya kukabidhiwa kitambulisho chake cha kupiga kura baada ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo. Picha na Freddy Maro.
Rais akuonyesha kitambulisho chake alichopewa mara baada ya kujiandikisha katika daftari daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo.
---
JUMLA ya watu milioni 11,248,194 wameandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura zoezi ambalo linaendelea kwa sasa hapa nchini likiwa limeingia mkoani Pwani.

Hayo yalisemwa leo kwenye Kijiji cha Msoga kata ya Msoga wilayani Bagamoyo na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa Damian Lubuva alipokuwa anampa taarifa Rais Dk Jakaya Kikwete mara baada ya kujiandikisha.

Bw. Lubuva alisema kuwa malengo ni kuandikisha watu milioni 21 hadi 23 kote nchini mara zoezi hilo litakapokamilika kati ya Julai mwishoni au Agosti mwanzoni kama hakutatokea matatizo.

“Hadi sasa ni mikoa 11 inaendelea na zoezi ambayo ni Mwanza Shinyanga, Geita, Simiyu, Mara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro Morogoro na jana ulianza mkoa wa Pwani,” alisema Lubuva.

Aidha alisema kuwa changamoto zilizojitokeza ni za kawaida hasa kutokana na mfumo huu kuwa ni mpya kwani kila jambo jipya lina changamoto zake.

“Mfumo huu ni mpya hivyo lazima kuwe na changamoto za hapa na pale lakini zoezi linakwenda vizuri na tunaamini kuwa tutafanikiwa kama tulivyopanga,” alisema Lubuva.

Mkoa wa Pwani una jumla ya vituo 1,752 na mashine za BVR 932 ambapo kata ya Msoga kuna jumla ya vituo 17 zoezi hilo kwa mkoa wa Pwani lilianza jana na litamalizika Julai 20.

Ijumaa, 3 Julai 2015

NEC NA VIONGOZI WA VYAMA VYASIASA, WAJADILI MAADILI YA UCHAGUZI WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji  Mstaafu Damiani Lubuva akizungumza wakati wa mkuato wa kujadili maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani katika mkutano uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.
  Mkurugenzi wa uchaguzi, Julius Mallaba akizungumza leo katika mkutano wa kujadili maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani katika mkutano uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.
  Baadhi ya viongozi wa vyombo vya siasa wakifuatilia kwa umakini katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
 Kamishina wa Polisi, Mussa Ali Mussa akizungumza kuhusiana na usalama kipindi cha kampeni na uchaguzi mkuu katika mkutano wa kujadili maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani katika mkutano uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.
Katibu Mkuu wa chama cha Tanzania Labour Part(TLP), Nancy Mrikalia akichangia maada katika mkutano wa kujadili maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani katika mkutano uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.

Na Avila kakingo, Globu ya jamii.

TUME ya uchaguzi NEC wakishirikiana na viongozi wa vyama vya siasa wakutana kujadili maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ikiwa tunaelekea katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Mstaafu Damiani Lubuva, Kwenye ufunguzi wa mkutano wa tume na viongozi wa vyama vya siasa kuhusu maadili ya uchaguzi leo jijini Dar es Salaam. 

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Mstaafu Damiani Lubuva amesema kuwa kupiga kura ni haki ya msingi naya kikatiba kwa kira raia wa Tanzania hivyo uchaguzi unatakiwa uwe wa haki, uhuru, uaminifu na wakuaminika. 

Lubuva amesema kuwa maadili yanayojadiliwa yahahusu zaidi vyama vya siasa, wagombea wote, serikali pamoja na tume ya uchaguzi pia kila chama na wagombea wanatakiwa kuheshimu na kutekeleza sheria za uchaguzi, kanuni na maadili na sheria nyingine za nchi katika kipindi cha kampeni kuanzia siku moja baada ya uteuzi hadi siku ya uchaguzi Oktoba mwaka huu. 

Pia ametoa wito kwa wanasiasa wote kuwaelimisha wafuasiwao kuondoka vituoni nara baada ya kupiga kura ili kuepusha msongamano wa vitendo vingine vinavyoweza kuchochea kuvunjika kwa amani. 

Kwa upande wa jeshi la polisi wametoa wito kwa wagombea wote watakao wania nafasi mbalimbali wafanye kampeni zake kipindi wakati kuna mwanga na si usiku ili kuepuka matatizo mbalimbali yatakayojitokeza.

MTAZAMO MPYA: ZOEZI LA KUJIANDIKISHA KWA KUTUMIA MFUMO WA BVR LA...

Mtazamo Mpya: ZOEZI LA KUJIANDIKISHA KWA KUTUMIA MFUMO WA BVR LA...: Bwana Chatoni Rashidi Chatoni. Na Clarence Chilumba,Masasi.   Wananchi waishio katika Halmashauri ya Mji wa Masasi Mkoani Mtwara hii leo...

UANDIKISHAJI PWANI JULAI 7 2015, DAR ES SALAAM JULAI 17 2015

Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililoahirishwa katika Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa PWANI sasa litafanyika kuanzia Julai 7 kwa Mkoa wa PWANI na JULAI 16 kwa Mkoa wa Dar es Salaam   
    
Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi -NEC kwa vyombo vya habari imesema Mkurugenzi wa NEC, JULIUS MALLABA anawahamasisha wananchi wa mikoa hiyo kujitokeza kwa ajili ya kujiandikisha ili kupata sifa za kushiriki Uchaguzi Mkuu baadaye Oktoba mwaka huu. 
       
Aidha MALLABA amesisitiza kuwa watu wenye kadi za kupigia kura za zamani wanatakiwa kuwasilisha kadi hizo ili kurahisisha uchukuaji wa taarifa zao. 
 Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililoahirishwa katika Jiji la DSM na Mkoa wa PWANI sasa litafanyika kuanzia Julai 7 kwa Mkoa wa PWANI na JULAI 16 kwa Mkoa wa DSM

 Uboreshaji wa Daftari hilo kwa Jiji la Dar es Salaam na PWANI uliahirishwa kutokana na kuchelewa kwa vifaa vya uboreshaji kutoka mikoa mingine