Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililoahirishwa katika Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa PWANI sasa litafanyika kuanzia Julai 7 kwa Mkoa wa PWANI na JULAI 16 kwa Mkoa wa Dar es Salaam
Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi -NEC kwa vyombo vya habari imesema Mkurugenzi wa NEC, JULIUS MALLABA anawahamasisha wananchi wa mikoa hiyo kujitokeza kwa ajili ya kujiandikisha ili kupata sifa za kushiriki Uchaguzi Mkuu baadaye Oktoba mwaka huu.
Aidha MALLABA amesisitiza kuwa watu wenye kadi za kupigia kura za zamani wanatakiwa kuwasilisha kadi hizo ili kurahisisha uchukuaji wa taarifa zao.
Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililoahirishwa katika Jiji la DSM na Mkoa wa PWANI sasa litafanyika kuanzia Julai 7 kwa Mkoa wa PWANI na JULAI 16 kwa Mkoa wa DSM
Uboreshaji wa Daftari hilo kwa Jiji la Dar es Salaam na PWANI uliahirishwa kutokana na kuchelewa kwa vifaa vya uboreshaji kutoka mikoa mingine
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni