USIUZE KADI YAKO

USIUZE KADI YAKO

Focusradiotz

Alhamisi, 30 Julai 2015

NEC YAONGEZA SIKU NNE ZA KUANDIKISHA WAPIGA KURA JIJINI DAR ES SALAAM

Tume ya Uchaguzi (NEC) leo imetangaza kuongeza siku nne zaidi za uandikishaji wa wapigakura kwa kutumia teknolojia ya BVR baada ya idadi kubwa ya wakazi wa Dar es Salaam kuitikia wito wa zoezi hilo. 

 Awali zoezi hilo lilikuwa likamilike kesho, Julai 31, lakini sasa litaendelea hadi Agosti 4, mwaka huu ili kukabiliana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza kujiandikisha. 

Kwa mujibu wa chombo hicho chenye mamlaka ya kusimamia shughuli zote za uchaguzi nchini, hadi jana, zaidi ya wakazi 1,000,000 walikuwa wamekwishaandikishwa jijini Dar es Salaam. 

 Ikizingatia matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Nec inatarajia kuandikisha jumla ya wakazi zaidi ya 2.8 milioni wa jiji hilo lenye idadi kubwa ya watu nchini Tanzania. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva, hadi sasa jumla ya zaidi ya watu 18 milioni wamekwishajiandikisha wakati tume ilitarajia kuandikisha watu kati ya 22 milioni na 23 milioni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni