TUME YA
TAIFA YA UCHAGUZI
Mkurugenzi wa Uchaguzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ndug. Kailima Ramadhani na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Bi. Awa Dabo, wakitoa taarifa fupi kuhusu kituo cha huduma kwa wapiga Kura.
Mkurugenzi wa Uchaguzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ndug. Kailima Ramadhani na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Bi. Awa Dabo, Kwa pamoja wakikata utepe kama ishara ya kuzindua kituo cha huduma kwa wapiga Kura.
KITUO CHA MAWASILIANO CHA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
Kuelekea
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Tume imeandaa kituo cha Mawasiliano “Call Center” kituo
hiki kimeanzishwa ili kuweza kuwasaidia wadau wetu wa Uchaguzi hasa Wapiga kura
kuweza kupata Elimu ya Mpiga Kura.
Wapiga
kura wataweza kuuliza maswali mbalimbali yahusuyo Uchaguzi Mkuu wa Rais,
Wabunge na Madiwani,
Ili
kuweza kupata huduma hii unatakiwa kupiga namba 0800782100 bure na kuuliza maswali yako au kutoa taarifa yeyote
kuhusu mwenendo wa Uchaguzi Mkuu.
Saa za Huduma
· Kuanzia tarehe 12-18 Oktoba
2015 kituo kitafanya kazi kuanzia saa 2:00 Asubuhi hadi saa 12:00 Jioni
· Kuanzia tarehe 19-30 Oktoba
kituo kitafanya kazi kwa saa 24
Taarifa za simu zilizopokelewa
kuanzia tarehe Oktoba 12, 2015
Jumla
simu 444 zilipokelewa tarehe
12/10/2015 na jumla simu 937
zilipokelewa tarehe 13/10/2015.
Tume
inawaomba waandishi wa habari na wadau wengine kuisaidia Tume kutangaza namba
hii 0800782100 ili wapiga kura
waweze kupata taarifa mbalimbali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni