TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH: UWEKAJI WAZI DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA MKOA WA DAR ES SALAAM
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
imekua ikiendesha zoezi la Uwekaji wazi Daftari la awali la Wapiga Kura katika
Mkoa wa Dar es Salaam.
Zoezi hili ambalo lilianza tarehe
19 Agosti, 2015 linatarajiwa kumalizika Tarehe 07 Septemba 2015
Daftari la awali la Wapiga Kura
limewekwa wazi katika kata zote za jiji la Dar es Salaam. Mashine za BVR zinazotumika kufanyia
marekebisho zimewekwa katika kata zote za jiji la Dar es Salaam.
Uwekaji
wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura unahusisha mambo yafuatayo:
· Kurekebisha
taarifa za Mpiga Kura zilizokosewa wakati wa uandikishaji.
· Kutoa
kadi mpya kwa wapiga kura waliopoteza kadi zao na wamo katika Daftari la awali
la Wapiga Kura.
· Kuondoa
Wapiga Kura waliofariki au waliokosa sifa kwa mujibu wa sheria.
· Kuhamisha
taarifa za wale waliohama toka Kata au Jimbo kwenda Kata au Jimbo lingine.
· Kutoa
nafasi kwa wapiga kura walioandikishwa kukagua taarifa kama zipo kwenye
Daftari.
· Wale ambao
wana kadi za Mpiga Kura lakini majina yao hayaonekani katika Daftari la Awali
la Wapiga Kura watafanyiwa uhakiki katika mifumo ya BVR na iwapo itathibitika
kuwa wamo watarudishwa katika mfumo wa Daftari.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
inategemea ushirikiano wenu katika kufanikisha zoezi hili kwa kuwafahamisha
wananchi ratiba ya zoezi hili na kuwahamasisha ili waweze kujitokeza kwa wingi
NB: Unaweza
kukagua taarifa zako kwa njia ya simu kwa kubonyeza *152*00≠ au tovuti www.nec.go.tz
na kufuata maelekezo
Kailima,
R. K
MKURUGENZI WA UCHAGUZI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni